Special Effects Mkeup ni sanaa inayotumia rangi na Prosthestics (vitu vinavyo bandikwa kwenye ngozi mfano vinyago 'MASK')
Katika kupaka au kubandika vitu kwenye ngozi ya mhusika ambaye anaweza akawa ni msanii wa maigzo ya jukwaani au filamu au mwanamitindo; Basi upakaji wako utaingiliana na ngozi na ndipo unapokuwa mpaka katu ya ngozi na kile ulicho kiweka juu ya ngozi ambapo inaweza ikawa rangi au Mask.
Kama tujuavyo sanaa ni kama WIZI! Naam ni wizi ndio kwani unamwongopea mtu mzima kwamba mhusika wako ameumia kumbe ni mzima kabisa bali ile kazi ya sanaa uliyoifanya juu ya ngozi ndio itakayo mfanya mtazamaji wako aamini kwamba ni kweli. Kwahiyo kama unaamua kuiba basi hakikisha unanyata kweli na sio unavaa SKUNA halafu unakwenda kuiba sehemu yenye Marumaru (Tiles)
Naweza toa mifano mingi lakini kikubwa ninacho kizungumzia hapo ni 'BLENDING' ambayo inamaanisha Mixing two things together. Yaani kuchanganya vitu viwili kwa pamoja. Lakini kwenye makeup ni kwamba sio tu kuchanganya vitu viwili kuwa pamoja, bali ni kuchanganya vitu hivyo bila kuwepo mpaka katikati ya hivyo vitu viwili ambavyo ni ngozi na makeup mfano ni mchoro hapo chini
Huu ni mfano wa mchanganyiko wa rangi mbili bila kujua mpaka ulipo na ndio hasa unahitajika kwenye makeup.
Mfano wa mchanganyiko usio hitajika katika makeup ni kama huu hapo chini ambapo hadhira akitazama anajua kwamba kazi yako ya sanaa haina uhalisia kwani anaona ni wapi makeup yako imeanzia na imeishia wapi kwahiyo hapo utashindwa kumwongopea mtu mzima na wakati mwingine hata mtoto pia kwani ni dhahiri mtu atajua mpaka umeanzia wapi tofauti na hapo juu.
Huu ndio mfano wa mpaka unaoonekana dhahiri bila kifichao.
Kwa maelekezo zaidi kuhusu somo hili unaweza kupiga +255716950845.


No comments:
Post a Comment