NJIA NZURI ZA KUJIFUNZA SPECIAL MAKEUP EFFECTS
Kwa wakati huu tushukuru kwanza uwepo wa You Tube na baadhi ya mitandao kama Instagram na mitandao mingine ya kijamii ambako wasanii wengi huweka kazi zao na baadhi ya walio bobea huweka mafunzo ya hatua baada ya hatua (Tutorial)
Kama unataka kujifunza wewe binafsi unaweza kutumia njia hizi na unaweza ukawa zaidi ya unavyo fikiria katika ulimwengu wa SPECIAL MAKEUP EFFECTS
1. Mtandao hasa You Tube Ndio Rafiki Yako
Mitandao imebadilisha ulimwengu wa Makeup kwa ubora. Kipindi cha nyuma watu iliwalazimu kuhudhulia Shule au Vyuo vya Mapambo na Urembo ili kujifunza na kuwa wabobezi . Lakini kwa siku hizi hata mtu ukiwa na Smart Phone au Computer basi unaweza kuwafikia wataalamu wa Makeup eidha kwa Blog au kwa mafunzo ya hatua kwa hatua kupitia You Tube (Tutorials)
Kuna watu mbalimbali wenye Makeup za kushangaza ulimwengu na hawana uchoyo bali huonesha wazi wanachokifanya kupitia You Tube na hudumia njia ambazo mtu yeyote anaweza kuelewa japo maranyingi hutumia Lugha za kigeni na hasa Kiingeleza kwahiyo itakuwa ni vyema pia kama unaelewa lugha hiyo au kama huelewi basi jaribu kusoma English Course ili uende nao sawa.
2. Wekeza kwenye Vifaa na Bidhaa Sahihi
Effects nyingi huweza kufanywa kwa vipodozi vya kawaida, Kwa mfano Rangi ya Dark blue, Brown na Purple zinaweza kutumika katika kuweka mfano wa damu kuvilia endapo mtu kapigwa na ngumi au kitu kingine endapo utajua nia sahihi ya kufanya kama inavyoonekana katika picha hapo chini.
Lakini changamoto ipo kwenye baadhi ya vitu wanavyotumia katika MAKEUP KIT (Visanduku vya vifaa vya makeup) ni kwamba baadhi ya vifaa havipo Tanzania kwahiyo itakulazimu kuagiza kutoka nchizao hadi kufika Nchini. Lakini Shtuka Fx Academy tuna baadhi ya Vifaa tunavitengeneza wenyewe kwa kuchanganya vitu mbalimbali na unaweza kuvipata na kuwasiliana nasi kwa +255716950845. Na vifaa vingine ni kwamba tumechunguza na kuona vipo katika jamii zetu japo vingine ni hatari kwa afya ya binadamu endapo vitatumika tofauti na masharti yake hasa kwa matumizi ya sehemu Nyeti kama vile Macho, Pua, Mdomo, Masikio na sehenu zenye Ngozi laini au kwa akina dada wanaotumia mkorogo. Unapotumia rangi mbalimbali kama damu basi kuwa makini rangi hiyo isije kuingia machoni au unapomwekea mtu mdomoni hakikisha iko katika hali ya usalama na usafi na inashauriwa kwa rangi za kumwekea mtu mdomoni ni bora zaidi kutumia rangi za chakaula mfano rangi za ubuyu.
3. Ingia Darasani
Endapo utaona You Tube Tutorials hazijakufundisha na wala huelewi chochote basi unakaribishwa katika darasa la Shtuka ili uweze kujifunza zaidi na kuendeleza ukipendacho. Kama upo kwenye mij mikubwa kama Los Angels na New York basi una bahati, Kuna madarasa mengi sana na kuna walimu wa kutosha waliofundisha watu wengi na wengi wao ndio wnafanya kazi kwenye televisheni na filamu mbalimbali za Hollywood
4. Siri ya Mafaniko ni Mazoezi
Mafanikio katika sanaa yoyote hutegemea mazoezi unayofanya mara kadhaa upatapo nafasi katika muda wako. Unatakiwa kuwatumia marafiki au ndugu wa karibu kwaajili ya kuwapaka na kuwachora muda wowote unapo pata wazo jipya au pia unaweza kujifanyia wewe mwenyewe kwa sehemu unayojiona kirahisi au unaweza pia kutumia kioo
Kadri unavyo jaribu kufanya mazoezi ndivyo jinsi unavyojiimarisha zaidi na kuwa Special Maeupist mzuri. Pia ni vizuri kuanzisha akaunti ya Instagram na Facebook au hata You Tube ili kuonehsa kazi zako na pia kupata muunganiko na watu waliopo katika tasnia ya filamu. Na hii itakusaidia kupata maoni mbalimbali yatakayo kujenga na pia utapata kukutana na watu wanaofanya kazi kama yako na kubadilishana nao mawazo na pia unaweza pata kazi kirahisi. Kumbuka kuwafollow walio katika tasnia ya filamu na kuomba urafiki kwa waongozaji wa filamu na pia kujiunga na magroup ya sanaa ili kusambaza kazi zako kwa picha na video ili kuendelea kukusanya maoni na ushauri.
5. Jitengenezee Mazingira ya Kazi
Kama utakuwa umesha fanya majaribio kwa mwili wako na kwa ndugu na rafiki zako na ukaona yako vizuri na kwa maoni mbalimbali uliyopata kutoka kwenye mitandao ya kijamii; Sasa hakikisha unashiriki kufanya makeup zako kwenye filamu.
Hapana, Simaanishi kwamba ukwee pipa uende hadi Marekani na kufanya filamu ya bajeti kubwa bali naamaanisha katika miji yetu huwa kuna kazi ndogondogo za machipukizi ambao huwa ndio wanaanza kuingia katika tasnia. Waandaaji hao maranyingu huwa hawana pesa za kuwakodi watu wa makeup walio bobea. Maranyingi watu hawa hutafuta watu ambao wanataka kufanya nao kazi kwa malipo madogo au hata bure kabisa. Japokuwa hutoweza kuongeza kipato lakini kwa kuanza unaweza ukajitengeneza mazingira ya kupata kazi nyingine siku za usoni endapo kazi hiyo itatoka au kuonekana. Pia usisahau kuandaa mikataba kwaajili ya makubaliano ya kazi utakayokuwa unafanya na mteja wako; Kwa kufanya hivyo utalinda haki yako ya msingi ufanyapo kazi na baada ya kazi.
FURAHIA FANI YAKO MPYA!


No comments:
Post a Comment